WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC leo wanafuta dhana kuwa Toto African ni tawi na mashabiki wa kufa na kupona wa Yanga kwa kucheza mechi ya kirafiki yenye kuanzia saa 10:00 uwanja wa CCM Kirumba.
Lengo la mchezo huo ni kuwapongeza 'Wanakishamapanda' kupanda ligi kuu msimu ujao.
Afisa habari wa Simba, Hajji Manara amesema: "Angalieni maslahi ya wananchi wa Mwanza, Toto isiangalie ushabiki wa Simba wala Yanga, wajikite kuiandaa timu, leo tunatarajia mchezo mgumu na ushindani".
"Niwaombe kocha wa Toto Tegete (John) kushikama na Wanamwanza ili kupandisha hadhi ya timu hiyo na soka la Mwanza"
Kwa upande wake kocha wa Toto, John Tegete amesema:
"Nafurahi Simba kutukubalia kucheza mechi ya kirafiki, tulikuwa mapumziko, lakini nikawaita wachezaji waje, tunatarajia ushindi leo".
Simba wapo Mwanza kwa siku ya pili wakitoka Rorya Mara walipokwenda kucheza bonanza na kufungua tawi la klabu hiyo.


0 comments:
Post a Comment