Monday, April 6, 2015


KUTOKA mwaka 2010/2011 Simba na Kagera zimekutana mara 10 baada ya leo kuchuana katika uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Katika mechi hiyo kali ya ligi kuu soka Tanzania bara, Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Ramadhani Singano kabla ya Rashid Mandawa kufuta bao hilo, lakini Mnyama alifunga goli la pili kwa penalti kupitia kwa mtaalamu wa mikwaju hiyo, Ibrahim Hajibu 'Mido'.
Katika idadi ya mechi 10 walizocheza sasa kutoka 2010, Simba wameshinda 3, wamefungwa 2 na kutoka sare 5.
Kagera wao wamefungwa 3, wameshinda 2 na sare 5.

REKODI ZA SIMBA NA KAGERA SUGAR KUTOKA 2010.

Wamekutana mechi 10 na katika mechi hizo ni mechi moja tu ambayo haikuwa na goli kwa timu zote. Ilikuwa ni Machi 27 mwaka 2011 ambapo Simba wakiwa uwanja wa Taifa walitoka 0-0.
Katika mechi nyingine zote, magoli yalikuwepo, iwe ni upande wa timu moja au zote.

MSIMU 2010/2011

Mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Kaitaba,Oktoba 27 mwaka 2010, Kagera walilala 2-0 na waliporudiana uwanja wa Taifa machi 27, 2011 Simba wakalazimishwa suluhu.

MSIMU 2011/2012

Mechi ya raundi ya kwanza ilipigwa septemba 18 mwaka 2011 uwanja wa Kaitaba na kushuhudia Kagera Sugar ikitoka sare ya 1-1 na Simba. Mechi ya raundi ya pili ilipigwa Taifa,  Simba walishinda 3-1.

MSIMU 2012/2013

Mechi ya kwanza ilipigwa uwanja wa Taifa Oktoba 17, 2012 na Simba walilazimishwa sare ya 2-2 na mechi ya marudiano ikapigwa Kaitaba aprili 25 mwaka 2013 na Kagera wakashinda 1-0.

MSIMU 2013/2014

Mechi ya kwanza ilipigwa Oktoba 30, 2013 uwanja wa Taifa na timu hizo kutoka sare ya 1-1. Mechi ya pili timu hizo zikatoka sare nyingine ya 1-1, Aprili 5 mwaka 2014 uwanja wa Kaitaba.

MSIMU 2014/2014

 Desemba 26 mwaka 2014 Kagera walishinda 1-0 uwanja wa Taifa na leo mechi ya pili msimu huu wamelala 2-1 uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Ukiangalia rekodi hizi, kwa miaka mitano sasa, Simba hakuwahi kushinda kwa matokeo ya 2-1 zaidi ya idadi nyingine ya magoli.

Kutoka katika ushindi wa 2-0 msimu wa 2010/2011 mpaka leo hii, Simba hawajawahi kushinda kanda ya ziwa dhidi ya Kagera.
Kumbuka kutoka mwaka huo Simba wamecheza mechi 4 uwanja wa Kaitaba, wakishinda 1 ambayo ndio nimetaja hapo juu, Wamefungwa 1 na kutoka sare 2.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video