Kimwaga ambaye kwa sasa ameshaanza mazoezi na timu yake baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kufuatia kufanyiwa opareshi ya goti nchini Afrika kusini mwaka jana, juzi jumamosi ya pasaka alipokea ubatizo na kipa imara katika kanisa la Katoliki Mbande Kigango cha Mbande.
Kimwaga ameuambia mtandao huu kuwa kwa muda mrefu alikuwa akipokea mafundisho kwa ajili ya ubatizo na kumunio ya kwanza.
Nyota huyo mwenye mipango ya kurejea uwanjani kwa kasi ameongeza kuwa baadhi ya marafiki zake, Frank Domayo, Kelvin Friday, vijana wa akadeni ya Azam fc na wageni wengine mbalimbali waalika walihudhuria siku hiyo muhimu katika maisha yake ya kiroho.
"Kikubwa namshukuru Mungu kwa kunipa uvumilivu na kufanikisha kitu hiki muhimu katika maisha yangu". Amesema Kimwaga.
Kimwaga alinyuka suti kali mno, kama humfahamu unaweza kudhani ni mchungaji au mbunge mtarajiwa. Wachungaji na Wabunge vazi la suti ndio rasmi kwao.
Joseph Kimwaga (kulia) akiwa na rafiki yake na mchezaji mwenzake wa Azam fc, Frank Raymond Domayo katika sherehe yake ya ubatizo na kipa Imara.






0 comments:
Post a Comment