Baada ya Simba kupoteza mchezo wa juzi Jumamosi dhidi ya Mbeya City kwa mabao 2-0, kipa wa timu hiyo, Peter Manyika, ameomba kuachwa kwa kile kinachodaiwa kushuka kiwango chake kwa sababu ya mrembo anayefahamika kwa jina la Nima.
Simba ambayo inaisaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ili msimu ujao iweze kushiriki michuano ya kimataifa, inaonekana kuanza kuikosa kwani kwa sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35 huku Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 42.
Manyika ambaye alidaka katika mchezo huo wa juzi, amechukizwa na matokeo hayo na kuamua kufunguka kwa kuandika ujumbe uliokwenda sambamba na picha ya mrembo huyo katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram akiomba kuachwa, ikiwa uongozi wa timu yake unahisi hafanyi vizuri katika kikosi hicho.
Ujumbe huo ulisomeka hivi: “Anayesema (mrembo) ananiua kiwango aje kudaka yeye sababu mimi siyo (tusi), nina haki ya kuwa na mpenzi kama watu wengine, mkihisi sifanyi kazi yenu mniache.”
Awali alipotafutwa kipa huyo na kusema kwamba hataki kusema chochote kuhusu hilo kwa sababu ameamua kuishi maisha yake binafsi, ndiyo maana amekuwa hafuatiliwi na watu.
Alipotafutwa baba yake kipa wa zamani wa Yanga, Manyika Peter ambaye alifunguka: “Unajua hiyo ishu bado sijaiona kwa sababu siku hizi nimekuwa sitembelei sana kwenye mitandao, lakini mimi kwake ni kama mshauri, hivyo ni vyema uongozi wa Simba uwe unakaa na wachezaji vijana kuwashauri mambo mbalimbali ambayo yatakuwa ni muongozo mzuri katika maisha yao.”

.jpg)
0 comments:
Post a Comment