Ligi kuu ya soka Tanzania bara inatarajia kuendelea tena hapo kesho ambapo kutakuwa na mchezo mmoja utakapopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam kati ya Yanga na Stand United kutoka Shinyanga.
Yanga ambayo wikiendi iliyopita ilikuwa na mchezo mgumu kabisa wa kimataifa wa kombe la shirikisho dhidi ya waarabu wa Tunisia Etoile Du Sahel.
Akifanyiwa mahojiano na kituo cha radio cha EFM Mkuu wa idara ya mawasiliano ya Yanga Jerry Muro amesema kuwa kuwa wao wapo vizuri kabisa kuhakikisha wanashinda mchzo huo wa kesho.
Muro aliendelea kusema kuwa wao watahakikisha kwamba wanashinda michezo mitatu ijayo ili waweze kutawazwa mabingwa na kuachana na mbilinge mbilinge za ligi hii ili kuangalia michezo yao ya kimataifa
"Kwa sasa atakayekuja mbele yetu tunachinja tu, chukua tarehe ya kesho halafu gawanya kwa mbili, utapata idadi ya magoli tutakayowafunga Stand United, kwa hiyo hata yakiwa magoli angalau basi kumi sio mbaya pia"
Alipoulizwa mbona walishindwa kuwafungwa Etoile idadi ya magoli kwa mujibu wa tarehe, Muro alijibu kuwa, Waarabu hao kutoka Tunisia walichungulia kidogo mambowanayozifanyia timu za hapa nchini na kujizatiti ili nao wasije kuaibika.


0 comments:
Post a Comment