Thursday, April 2, 2015


Na Bertha Lumala, Shinyanga
Ama kweli majuto ni mjukuu! Baada ya kuwaona wa nini, na Mtibwa Sugar FC na Azam FC zikawanasa, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm, ameuagiza uongozi wa Yanga SC kuhakikisha unawarejesha kundini beki wa pembeni kushoto David Luhende na mshambuliaji Didier Kavumbagu.

Pluijm raia wa Uholanzi, amekaririwa na mmoja wa mitandao ya kimataifa ya michezo akieleza kuvutiwa na wachezaji hao ihuku akiagiza uongozi wa wanajangwani uhakikishe unawarudisha ili kuimarisha kikosi chake ambacho amegundua kina upungufu kwenye sehemu ya ulinzi na ushambuliaji.

“Ninataka kuimarisha kikosi changu kwa sababu malengo yetu msimu ujao ni kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi kwenye ligi ya ndani na hata kwenye michuano ya kimataifa na wachezaji hao ndiyo sahihi kutokana na kuelewa vizuri mazingira ya timu,” amesema Pluijm.

Wachezaji hao waliondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita, Kavumbagu alisema sababu iliyomuondoa ni kutojua mstakabali wake baada ya mkataba wake kumalizika na uongozi kuwa kimya lakini Luhende viongozi waligoma kumuongeza mkataba kwa sababu kiwango chake kilionekana kushuka.

Luhende amekuwa nguzo muhimu kwa mafanikio ya Mtibwa Sugar FC msimu huu huku Kavuambagu akiwa kinara wa mabao Azam FC na kukamata nafasi ya pili kwa wafumania nuavu hatari Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao 10, moja nyuma ya kinara Simon Msuva wa Yanga SC.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video