Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
"Mbinu bora ya kujilinda si kupaki basi, ni kucheza kwa kushambulia." Ni kauli ya Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro', aliyoitoa kuelekea mechi yao ya keshokutwa dhidi ya FC Platinum nchini Zimbabwe.
Cannavaro amekaririwa katika mahojiano na moja ya vituo vya redio jijini hapa leo asubuhi akitamba kuwa Yanga SC itaibuka na ushindi tena dhidi ya wapinzani wao hao katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.
"Mbinu bora ya kujilinda si kupaki basi, ni kucheza kwa kushambulia. Yanga inakwenda Zimbabwe kushinda tena kama ilivyofanya hapa nyumbani. Wachezaji tuna ari kubwa ya kushinda ugenini na nina matumaini makubwa tutafanya hivyo," ametamba Cannavaro.
Nahodha huyo wa Yanga SC, Taifa Stars na Zanzibar Heroes, amesema kikosi chao kimefanya mazoezi ya mwisho leo kwenye Uwanja wa Karume jijini hapa na kitaanza safari ya kwenda Zimbabwe kesho asubuhi.
Dk Jonas Tiboroha, Katibu Mkuu wa Yanga SC, amesema msafara wa mabingwa haoa mara 24 wa Tanzania Bara, utakuwa na nyota 20 na viongozi 10.
Dk Tiboroha amesema washambuliaji Mliberia Kpah Sherman na mzaliwa wa Mwanza Jeryson Tegete pamoja na kiungo fundi kutoka Brazil, Andrey Coutinho watabaki jijini hapa wakati timu ikipaa kwenda Zimbabwe kutokana na kile kilichoelezwa na Juma Sufian, daktari wa Yanga SC, kwamba wana majeraha.
Kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na kocha mkuu Mdachi Hans van der Pluijm na msaidizi wake Boniface Mkwasa, kilishinda mabao 5-1 dhidi ya FC Platinum katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini hapa mwezi uliopita.
Endapo Yanga SC ikifanikiwa kuwatoa Wazimbabwe hao, itakutana na mshindi kati ya Etoile du Sahel FC ya Tunisia na Benfica de Luanda FC ya Angola katika hatua inayofuata ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Etoile ambayo mwaka juzi ilimnunua kiungo mshambuliaji wa Simba SC kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, kwa mali kauli ya dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 450), ilishinda 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Tunis, Tunisia mwezi uliopita.

0 comments:
Post a Comment