Nyoso (kulia) alifanya kazi nzuri kumzuia Ibrahim Hajibu siku waliposhinda 2-1 dhidi ya Simba mwaka hu
BEKI mahiri na mkongwe wa Mbeya City fc, Juma
Nyosso amesema hakuna kulaza damu, huu ni muda wa kazi, mambo mengine ni kuweka
pembeni.
Januari 28 mwaka huu Mbeya City iliifunga Simba
mabao 2-1 uwanja wa Taifa Dar es salaam, lakini Nyoso alifanya tukio la aina
yake ikimpapasa makalio mshambuliaji wa Simba, Elius Maguli.
Baada ya tukio hilo kubainika siku chache
zilizofuata, Nyoso alifungiwa mechi 8 na mechi ya kwanza kucheza baada ya
kifungo hicho ilikuwa dhidi ya Azam waliyotoka 1-1 na Azam fc uwanja wa Azam
Complex katikati ya wiki iliyopita.
Kuelekea katika mechi hiyo, Nyoso amesema ni wakati
mwingine mzuri wa kuwaonesha Simba kuwa yeye ni beki mgumu.
“Simba hakika nitawazuia kwa kushirikiana na
wenzangu, wana wachezaji wasumbufu kama Okwi (Emmanuel), Hajibu (Ibrahim) na
wengine, lakini nimejipanga kumficha hasa Okwi ambaye ni mtu hatari”. Amesema
Nyoso.
Baada ya Okwi kuambiwa tambo hizo amejibu kuwa: “Ligi
ni ngumu, wapinzani wananikamia, lakini siku zote natafuta mbinu mpya za
kuwatoka. Niko tayari kupambana kwa ajili ya timy yangu ya Simba”.
Nyoso amewahi kuichezea Simba siku za nyuma na
Coastal Union uliopita alikuwa Coastal Union.


0 comments:
Post a Comment