Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amewaka na kusema kuwa kujiangusha kwa Ander Herrera katika dakika za mwisho za mchezo wa jana kati ya Chelsea na Man U itasahaulika mapema zaidi kwa kuwa ni mchezaji wa Man United.
Kocha huyo Mreno amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakitendewa tofauti kabisa na wachezaji wa timu nyingine katika msimu wote huu wa ligi kuu nchini Uingereza.
Baada ya Herrera kuzawadiwa kadi hiyo ya njano, Mourinho amesema kuwa mpaka sasa tukio hilo hata halijazungumziwa kama ambavyo lingezungumziwa endapo angekuwa ni mchezaji wa Chelsea.
"Nina furaha sana kwa kuwa safari hii haikuwa mchezaji wa Chelsea kwa sababu, laiti kama ingekuwa ni mchezaji wa Chelsea, yaani ndani ya Sky Sports ungesikia huyu ni muongo tu," Mourinho aliwaambia waandishi.
"Lakini kwa sababu ni mchezaji wa Man United, kamwe hautasikia mtu yeyote akilizungumzia hilo, ila mimi sina tatizo juu ya hilo. hakuna njama sasa; furaha yangu ni kwamba hakuwa mchezaji wa Chelsea."

0 comments:
Post a Comment