Sunday, April 19, 2015

Baada ya winga wa Chelsea Eden Hazard kufunga goli la pekee dhidi ya Manchester United katika dimba la Stamford Bridge jana Jumamosi, wachambuzi wa Sky Sports wamedai kuwa kabla ya goli hilo kufungwa kuna madhambi yalikuwa yamefanyika. 
Nahodha wa Chelsea John Terry alimfanyia madhambi mshambulizi wa Man United Radamel Falcao na kusababisha kudondoka chini.
Kiungo mchezeshaji wa Chelsea Cesc Fabregas aliuchukua mpira huo huo na kumpa Oscar na kuugonga kwa kisigino na kumpa Hazard ambaye alitiririka nao kabla ya kuuweka kimiani na kuwapa wenyeji goli la kwanza na la ushindi. 
Beki wa Chelsea John Terry akitokea nyuma na kumchezea madhambi mshambulizi wa Man U Radamel Falcao
Ukabaji wa Terry dhidi ya Falcao ulisababisha Falcao apoteze mpira na kuchukuliwa na Cesc Fabregas ambaye ndiye aliyeanzisha 'move' ya goli.
Thierry Henry, Jamie Redknapp na Graeme Souness wotekwa pamoja walikubaliana wakati wakifanya uchambuzi wa mchezo huo wakati wa mapumziko kwamba Terry alimfanyia madhambi Falcao. 
Souness alisema, 'alimuwekea kiwiko Falcao karibu na kichwa chake na hayo moja kwa moja ni madhambi.'
Nahodha wa zamani wa Arsenal Henry, naye alisema, namuonea huruma sana Falcao kama mshambuliaji mwenzangu. Alivyoulizwa kama angependelea uwe ni mpira wa adhabu, Henry alisema, 'ndiyo, tena mapema mno ingekuwa.'
Naye Redknapp alikiri vivyo hivyo na kusema kuwa ingekuwa vizuri zaidi kwa Falcao kama angedaka hata miguu ya Terry, mwamuzi angepuliza kipyenga tu wala asingeacha tukio liendelee, lakini hata hivyo kwangu mimi ile ilikuwa ni faulo tu.' 
Wachambuzi wa Sky  Sports Graeme Souness (kushoto), Thierry Henry (katikati) na Jamie Redknapp wote kwa pamoja walikubaliana kuwa Terry alimfanyia madhambi Falcao.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video