Sunday, April 12, 2015


YANGA SC leo jioni inacheza mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hii ni siku muhimu sana kwa mlinda mlango namba moja kwa sasa, Ally Mustapha Mtinge 'Bartez' ambaye anasherekea siku yake ya kuzaliwa.
Kama Yanga watashinda leo itakuwa faraja kubwa kwa kipa huyu aliyepitia misukosuko ya soka katika klabu za Simba na Yanga.
Alipokuwa Simba alikaa benchi sana na kumpisha Juma Kaseja na Deo Munish wakitumika.
Alipohamia Yanga wakakutana tena makipa hao watatu ingawa Kaseja ametimka, alianza kudaka, lakini mambo yakaharibika baadaye.
Toka mwaka huu uanze, Bartez amekuwa chaguo la kwanza na amecheza mechi zote za ligi kuu na michuano ya kombe la Shirikisho.
Kipa huyo ameonesha kiwango cha juu muda wote, licha ya kuwa na makosa ya kawaida ya kimpira.
Kheri yako ya kuzaliwa kipa wa  mabingwa mara nyingi za historia wa ligi kuu Tanzania bara.
Hongera kwa kutimiza miaka 31,tarehe kama ya leo, Aprili 12 mwaka 1984  ndipo Ally Mustapha Mtinge "Barthez alizaliwa.
Mwenye enzi mungu akupe maisha marefu zaidi na mafanikio katika kipaji chako cha soka.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video