Na Anwar Binde.
Kijana mmoja nchini Saudi Arabia alimpiga picha binti huyu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 akitafuta chakula katika pipa la taka taka kisha akaituma mitandaoni na kuweka maneno ya kuudhi yakiashiria kuwadhihaki mashabiki wa Club ya Al Ittihad ya jeddah kwasababu binti huyo alikuwa Al Ittihad na alimaanisha hapo ndipo wanapostahili kuwepo” .
Baada ya kuituma mitandaoni kijana huyo alipata shinikizo kubwa kutoka kwa jamii , siku chache baadaye kijana huyo aliamua kurudi kwa binti huyo kumuomba msamaha akiwa na zawadi kadhaa .
Tukio hilo limesababisha shabiki mmoja tajiri wa Club ya al Ittihad kujitolea dola 16,000 kumsaidia binti huyo sambamba na mwanamichezo maarufu nchini Saudi Arabia dereva wa magari ya mashindano Yazeedi Al Rajhi kujitolea zaidi ya dola 100,000 kusaidia familia ya bint huyo. Kijana huyo alirudi katika mitandao ya jamii kuomba msamaha akiambatanisha na picha aliyopiga mara ya 2 na bint huyo .
Hii ndio selfie aliyojipiga kijana huyo na binti akitafuta chakula kwenye jalala
Na hii ndio picha aliyopiga baada ya kuomba msamaha na kumpelekea zawadi




0 comments:
Post a Comment