Etoile Du Sahel wanajulikana kwa jina la utani kama " mashetani wekundu" au nyota ya jangwa la Sahara. Hawa ndio watakutana na timu ngumu Afrika mashariki na kati YANGA AFRICA .
Sahel ilianzishwa tarehe 11 may 1925 huko Tunisia na mahasimu wao wakubwa ni Timu ya Espearance du Sportivu . Ni wakongwe kihistoria ukilinganisha na Yanga iliyoanzishwa muongo mmoja baadae yaani 11 february 1935 jijini Dar. Wakati ligi ya ndani Yanga ni bingwa mara 24 , Waarabu hao wamebeba kombe la ligi ya ndani mara 9! tu. Mara ya kwanza walibeba mwaka 1950.
Kimataifa wababe hao wanaiacha Yanga mbali kidogo, Sahel pamoja na Juventus wapo katika historia ya FIFA kwa kushinda kombe la mabara huku wakishinda official cups zote za CAF na kwa mara ya kwanza waliitikisa Africa mwaka 1995.
Wanasifika kwa mechi za ugenini hivyo Yanga SC inabidi wawe makini sana. Wanakumbukwa sana na Al Ahly kwa matokeo ya 0_0 pale Tunis kabla ya kuwashangaza ndani ya Cairo kwa 3_0 na kubeba kombe.
Yanga nao si wa kubeza mbali ya kuwagonga Platinum 5_2 lakini wanakumbukwa kwa kuinyanyasa Sports Club Villa kwa kunyakua kombe ndani ya ardhi yao mara mbili. 1993&99.
Ingawa Sahel ni mabingwa wa michuano hii mwaka 1997 na 2003, Yanga chini Hans van der Pluijm itawashangaza kwa ushindi mnono. Kikubwa ni kujiamini na kufanya kazi.
Source: Samuel Samuel in Sports


0 comments:
Post a Comment