Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
STAND UNITED wamefanikiwa kushinda bao 1-0 katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwa siku mbili kuanzia hapo jana na leo
Bao la Stand United lilifungwa jana na Haruna Chonongo katika dakika ya 12' kabla ya pambano hilo kuvunjika dakika ya 33' kufuatia mvua kubwa kunyesha mjini Shinyanga.
Muamuzi wa mechi, Ahamad Simba amechezesha kwa dakika 57' zilizosalia asubuhi na mechi kumalizika kwa suluhu (0-0).
Kwa matokeo hayo Stand United wanafikisha pointi 24, pointi moja mbele ya Mtibwa wenye pointi 23.
Kwa matokeo hayo Stand United wanafikisha pointi 24, pointi moja mbele ya Mtibwa wenye pointi 23.
Hii mara ya pili msimu huu mechi moja kuchezwa mara mbili uwanja wa Kambarage ikiwahusishwa wenyeji Stand United.
Februari 28 mwaka huu mechi baina ya Stand United iliahirishwa kutokana na mvua kunyesha na wakati huo Stand walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Abasarim Chidiebele.
Siku ya pili asubuhi Chidiebele alifunga bao lingine na Stand kuibuka na ushindi mnono wa 2-0.
Mtibwa Sugar imepoteza pointi sita katika uwanja wa Kambarage kwani jumatano ya wiki iliyopita walifungwa 2-1 na Kagera Sugar.
Ligi kuu inaendelea kwa mechi moja kupigwa uwanja huu wa Kambarage ambapo wenyeji Kagera Sugar wanachuana na Simba SC.
Mechi hii inaoneshwa moja kwa moja "Live' na Azam TV kupitia chaneli ya Azam TWO kuanzia saa 10:00 jioni.
Awali mechi hiyo ilitakiwa kupigwa jumamosi iliyopita, lakini iliahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji kutokana na mvula zinazoendelea kunyesha.
Muda huu mjini Shinyanga kuja kijua kinawaka, lakini bado kuna wingu linaloashiria uwezekana wa mvua kama ilivyokuwa jana.



0 comments:
Post a Comment