Bondia Mada Maugo (kushoto) sasa ni meneja wa Thomas Mashali, 'Simba asiyefugika' (kulia)
Na Kassim Mtolea
WIKI chache baada ya kutangaza kuupa kisogo mchezo wa masumbwi hapa nchini bondia Thomas Mashali(Rais wa jela) ametengua kauli yake.
Hayo yamewekwa wazi na bondia mwenzake Mada Maugo alipokuwa akizungumza na MPENJA BLOG baada ya kuulizwa kuhusu maoni yake kufuatia taarifa ya Mashali kuachana na mchezo huo.
"Nimekaa chini na nimezungumza na Mashali na amekubali kurejea kwenye ndondi na kwa sasa mimi ndiye nitakuwa meneja wake na hivi karibuni kutakuwa na pambano nje ya nchi la Thomas"alisema Maugo anayependa aitwe mbunge wa Rorya.
Meneja huyo mpya amelizungumzia suala adhabu ambayo PST walimgonga Mashali nyundo ya miaka miwili
Amesema"Naamini watakuwa wamemsamehe ikizingatiwa kuwa Mashali hana chanzo chochote cha mapato zaidi ya masumbwi hivyo kumfungia ni kutaka kumuua njaa"
Alipoulizwa kuhusu deni la shilingi millioni moja ambalo Mashali anadaiwa na promota Juma Msangi,Maugo amesema suala hilo limekwisha na wawili hao wamekubaliana kulipana kidogo kidogo mpaka pesa zitakapokamilika.
Mashali alijiondoa kwenye mchezo wa ndondi baada PST kutangaza kumfungia baada ya kukacha pambano lake la tarehe 27 mwezi wa tatu dhidi ya bondia Karama Nyilawila.
Mtandao huu bado inaendelea kumtafuta katibu mkuu wa PST kujua zaidi kuhusu taarifa hizi .

0 comments:
Post a Comment