Friday, April 17, 2015


Na Kassim Mtolea, Shinyanga

JKTRuvu ni kama wamekubali matokeo ya mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara  dhidi ya Stand United unaopigwa leo uwanja wa CCM Kambarage,  mjini shinyanga.

Timu hiyo ya jeshi iliwasili jana alhamisi tayari kwa mchezo huo lakini wasiwasi ni juu ya uchovu wa kikosi cha maafande hao.
Msemaji wa Jkt Ruvu,  Constantine Masanja amesema wapo tayari kwa mchezo huo.
"Tulijua tuna mchezo jumamosi lakini tukapokea mabadiliko kwamba tunatakiwa kucheza ijumaa na sisi ni wanajeshi tukaanza safari na sasa tupo Shinyanga".
Alipoulizwa kama kutakuwa na visingizio kama watapoteza mchezo huo dhidi ya wapiga debe hao, Masanja amesema hana wasiwasi na vijana wake.
"Vijana wananyumbulika kwahiyo wako fiti kwa mchezo na hakuna kumtafuta mchawi hata tukipoteza mchezo wa leo"
Kwa upande wa stand kupitia mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Muhibu Kanu amewaomba watu wa Shinyanga na kanda ya ziwa kwa ujumla kutia ubani ili wapate ushindi leo.
"Timu iko sawa na tupo tayari kupamba nao lakini dua zao ni muhimu sana kwetu ili tupate ushindi nyumbani"alibainisha Kanu.
Timu hizo zinakutana leo kambarage uwanja ambao umekuwa hautabiriki kufuatia mara kwa mara kugeuka bwala la kufugia samaki kutokana mvua zinazoendelea mjini Shinyanga.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video