Friday, April 3, 2015


Danny Mrwanda (kulia) akiwa na Saimon Msuva kwenye moja ya mechi ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu ambayo alifunga goli moja katika ushindi wa 3-1.
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

'Kanuni za Ligi za TFF toleo la zinaweka wazi kwamba klabu za Ligi Kuu zinaweza kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi watano.'
  
Kila mtu na mtazamo wake! Wakati wachambuzi wengi wa soka nchini wameshauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liongeze idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu Tanzania Bara, mshambuliaji Danny Mrwanda wa Yanga SC amesema kitu tofauti.

Katika mahojiano na moja ya vituo vya redio jijini hapa, Mrwanda ambaye mpaka sasa amefunga mabao sita Ligi Kuu msimu huu, amesema kuna haja TFF kupunguza nyota wa kigeni Ligi Kuu ili kuwapa nyota wazawa.

Kutokana na uzoefu wake katika nchi za Vietnam na Kuwait, Mrwanda amesema ipo haja Tanzania kuachana na wachezaji wa kigeni ili kuwapa fursa wazawa kwa manufaa ya taifa.

"Mchezaji wa kigeni anapaswa kuwa mzuri kuzidi wazawa. Mathalani kama ni mshambuliaji, anatakiwa kufunga mabao mengi kuzidi washambuliaji wa ndani, lakini hili liko tofauti sana hapa kwetu (Tanzania). Wachezaji wa kigeni ni wa kawaida sana," Mrwanda amesema;

"Ninafikiri wapunguze kutoka watano hadi watatu au wanne na kuwe na kanuni inayozuia wasianze kwa pamoja katika mechi moja, waanze wawili.

"Kwa sasa (Simon) Msuva ndiye anayeongoza kwa mabao. Nilitegemea kuona nyota wa kigeni wakiwa na mabao 15 au zaidi kwa sababu mzawa anayo 11, lakini hali ni tofauti."

Mrwanda, mzaliwa wa Arusha, ambaye Jumatatu atatimiza miaka 32, anaunga mkono Azimio la Bagamoyo la 2007 linalotaka mpro wapunguzwe kutoka watano hadi watatu akiamini kufanya hivyo kutaboresha kiwango cha Taifa Stars.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video