MANCHESTER United itampatia Straika wake Mholanzi, Robi van Persie paundi milioni 5 ili aondoke klabuni hapo majira ya kiangazi mwaka huu.
Van Persie amebakiza miezi 14 katika mkataba wake, lakini United wapo tayari kumuuza na kufidia kuvunja mkataba wake ili wapate mshambuliaji mwingine.
Mdachi huyo mpaka sasa msimu huu amefunga magoli 10 tu.
Miamba ya Italia, Inter Milan na Juventus zinahusishwa kuiwinda saini ya nyota huyo mwenye miaka 31 anayelipwa paundi laki mbili na nusu Old Trafford


0 comments:
Post a Comment