JUMAMOSI ya wiki iliyopita, Yanga ilifuzu hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho kwa jumla ya magoli 5-2 dhidi ya timu ya Zimbabwe ya FC Platinum.
Yanga walifungwa bao 1-0 na wenyeji wao, lakini walikuwa na mtaji mkubwa wa mabao 5-1 waliyopata katika uwanja wa Taifa, februari 15 mwaka huu.
Ni nadra kutokea! kocha wa Yanga ambaye ni mwanachama wa klabu hiyo pia, Mholanzi, Hans van der Pluijm alionesha mapenzi makubwa na uzalendo kwa timu yake na Tanzania kwa ujumla kwa kujifunika bendera ya Taifa ya Tanzania kama,cheki picha.



0 comments:
Post a Comment