Monday, April 6, 2015


'Mtibwa Sugar FC, mabingwa mata mbili wa Tanzania Bara 1999 na 2000, wameongoza ligi kwa muda mrefu, lakini sasa wako nafasi ya tatu kutoka mkiani.'

HAKIKA Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ni ngumu! Hilo limethibitika kutokana na hali ya kikosi cha Mtibwa Sugar FC ambacho sasa kinapumulia mashine katika mbio za kuhakikisha hakishuki daraja msimu huu.

Baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Stand United FC mjini Shinyanga leo asubuhi, uongozi wa Mtibwa Sugar FC umesema timu yao imekumbwa na upepo mbaya katika ligi hiyo.

Msemaji wa Mtibwa Sugar FC, Thobias Kifaru, ameuambia mtandao huu kuwa sasa wanapambana kuhakikisha wanainusuru timu yao kuporomoka daraja.

"Tumekumbwa na upepo mbaya, kutoka kileleni mwa msimamo hadi kupigania kuporomoka daraja si mchezo. Timu yetu ni nzuri, lakini kuna upepo unaisumbua katika kipindi hiki," amesema Kifaru huku akiweka wazi kuwa watakaa kuangalia tatizo lilipo.

Mtibwa Sugar FC inayonolewa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime, ina pointi 23, tatu mbele ya timu iliyoko mkiani mwa msimamo, Tanzania Prisons FC ya Mbeya.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video