Monday, April 6, 2015



'Kagera Sugar FC, mabingwa wa Kombe la Tusker 2004, waliifunga Simba SC bao 1-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa Novemba mwaka jana.'

WANAJITETEA! Baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC katika mechi pekee ya leo ya Ligi Kuu ya Bara, benchi la ufundi la Kagera Sugar FC, limeibuka na kudai kuwa wapinzani wao wamebebwa na refa wa mechi hiyo.

Kocha mkuu wa Kagera Sugar FC, Mganda Jackson Mayanja, amesema muda mfupi uliopita kuwa Simba SC imebebwa na refa Erick Onoka.

"Tungeweza kushinda mechi hii, lakini refa alikuwa na matokeo mfukoni, kwani hata penalti waliyopewa Simba haikuwa halali," amesema Mayanja huku akiungwa mkono na msaidizi wake Murage Kabange ambaye pia amedai refa huyo kutoka Arusha ameinyonga Kagera Sugar FC makusudi.

Mbali na kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar FC jijini Dar es Salaam mzunguko wa kwanza, ushindi huo umeifanya Simba SC ifikishe pointi 35 moja nyuma ya mabingwa watetezi Azam FC wenye mechi tatu mkononi, hata hivyo.

Vikosi vilikuwa:

Kagera Sugar FC: Agaton Anthony, Erick Murilo, Salum Kanoni, Erick Kyaruzi, Geroge Kavila, Malegesi Mwangwa, Juma Mpola/Paul Ngwai, Babu Ally, Rashid Mandawa, Atupele Green na Adam Kingwande. 

Simba SC: Peter Manyika, Nassor Masoud, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Awadh Juma, Ramadhan Singano, Said Ndemla, Dan Sserunkuma, Ibrahim Ajibu na Emmanuel Okwi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video