Sunday, April 5, 2015


SIMBA, Yanga ni klabu kongwe zaidi nchini na hakuna shaka kwamba zimeleta mchango mkubwa kuendeleza soka la nchi hii.
Kwa upande wa pili zinalaumiwa sana kuharibu soka hasa kwa vitendo vyao vya kuua vipaji vya wachezaji.
Kuna mifano mingi ya wachezaji waliomalizia soka lao la ushindani katika klabu hizi mbili kwa kukosa namba au kuachwa baada ya kupata majeruhi, sina haja kutoa mifano kwa kila mtu anajua.
Oktoba 20 mwaka 2013, Simba na Yanga zilitoka sare ya 3-3. Hii ni mechi iliyoleta matokeo ya ajabu katika mechi za watani hawa wa jadi.
Yanga chini ya kocha Ernie Brandts walianza kufunga magoli kipindi cha kwanza na wakacheza kwa mbwembwe huku akina Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa  wakituliza mipira kwa magoti na kupiga pasi kwa visigino.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa magoli 3-3. Kocha wa wakati huo wa Simba, Abdallah Kibadeni aliwatuliza vijana wake vyumbani na kuwataka kupambana, walirudi na kusawazisha magoli yote.
Ilikuwa mechi kali iliyosababisha watu wengi kuzimia uwanjani na wengine kupoteza maisha. Baada ya matokeo hayo, kila timu ilitoa kafara watu inawashutumu kufanya uzembe.
Yanga waliaanza na Golikipa Ally Mustapha 'Bartez'. Alilaumiwa kufungisha na kuhujumu timu. Kwa bahati mbaya, Bartez alitokea Simba.
Baada ya tukio hilo, Bartez alikuwa mnyonge na aliharibikiwa kisaikolojia na kuanza kuchoma mahindi benchi huku akiwaona Juma Kaseja na Deo Munishi 'Dida' wakicheza.
Baadaye Kaseja naye mambo yakamdodea baada ya kufungwa mechi ya nani mtani Jembe magoli 3-1, hususani bao la Awadh Juma liliwachukiza wengi. Kwasababu Juma alitoka Simba, basi muendelezo wa shutuma ukaendelea.
Alikuja kufungwa goli la Kizembe Morogoro na huko tanga Yanga ikichapwa 2-1 na Mgambo JKT, hakika hapo ndipo Kaseja ukawa mwisho kuichezea Yanga.
Licha ya umahiri wake wa kudaka, hakuaminiwa tena, akaanza kukaa benchi na Bartez huku wakimuacha Dida anatamba.
Dida alionesha kiwango cha juu kwa muda wote, alikosekana tu pale alipokuwa majeruhi. Msaidizi wake akawa Juma Kaseja kwa mbaali.
Kwa habati mbaya mpira huwezi kuwa katika kiwango chako kwa muda wote, Dida kuna kipindi alianza kufungwa magoli ya kizembe na watu wakaamusha maneno kama kawaida.
Desemba 28 mwaka jana, Didier Kavumbagu na John Bocco walimtungua Dida katika sare ya 2-2 na Azam fc. Mashabiki wa Yanga walichukizwa na kiwango cha chini cha Dida siku hiyo.
Siku chache baadaye alipata majeruhi baada ya kuchanwa na bati akiwa nyumbani kwake na akatoa mwanya kwa Kaseja kucheza baadhi ya mechi, huku Bartez akiendelea kujutia sare ya 3-3.
Alipokuja Marcio Maximo katikati ya mwaka jana, aliendelea kumuamini Dida, huku Bartez na Kaseja wakiendelea kukaa benchi.
Maximo alitimuliwa kazi desemba mwaka jana baada ya kufungwa 2-0 na Simba katika mechi ya nani Mtani Jembe.
Alipokuja Hans van der Pluijm alimtumia Dida katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Azam fc desemba 28 mwaka jana.
Dida alifungwa goli la kizembe na Didier Kavumbagu na akafungwa lingine la kichwa na John Bocco. Hapo Yanga wakaanza maneno kwamba ameshuka kiwango.
Yanga ilipoelekea kombe la Mapinduzi, kocha Pluijm akaanza kumjaribu Bartez huku Kaseja akiendelea kusugua benchi ambaye baadaye aliamua kuachana na Yanga.
Bartez alicheza vizuri kombe la Mapinduzi ingawa Yanga ilitolewa robo fainali. Bartez alionekana kuwa na hofu golini, hajiamini, lakini kadri alivyoendelea kucheza aliendelea kuimarika na kurejesha hali yake ya kawaida baada ya kusotea benchi.
Baada ya hapo akajimilikisha namba na amecheza mechi zote za ligi kuu toka mwaka huu uanze na mechi nne za kombe la shirikisho.
Alipangwa kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya BDF XI ya Botswana na kucheza vizuri, akapangwa kwenye kipigo cha 2-1 walichopa Yanga mechi ya Marudiano Botswana, hata hivyo alicheza vizuri mno.
Baada ya mechi hizo, Yanga wakakumbana na kipigo cha 1-0 dhidi ya Simba katika mechi ya ligi machi 8 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Bartez alifungwa goli la mbali na Emmanuel Okwi kwa kosa la kuingia kutoka golini bila sababu. 
Matokeo yaliwaumiza Yanga kama unavyojua mechi ya mtani wa jadi. Mengi yakaaibuka, baadhi wakawa wanawatuhumu baadhi ya wachezaji hasa waliotokea Simba enzi hizo wakidai ni virusi.
Bartez alilaumiwa kwa uzembe, lakini haikuwa kama kipindi kile cha 3-3. Hii ilichangiwa sana na Yanga kuwa na mechi ya raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho dhidi FC Platinum.

Dida
Katika ushindi wa 5-1 uwanja wa Taifa machi 15 mwaka huu, Bartez alikaa golini na kufanya kazi nzuri. Jana katika mechi ya marudiano Yanga wakifungwa 1-0, Bartez ndiye alikuwa nyota wa mchezo.
Alifanya kazi iliyotukuka kwa walioshuhudia mechi kupitia Azam TV ni mashahidi.
Alidaka na kuonesha maajabu ya kuokoa, mashuti ya karibu ya washambuliaji yaliishia mikononi na miguuni mwake.
Yanga walisonga mbele kwa matokeo ya jumla ya 5-1 na sasa wanabarizi hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho.
Ally Mustapha Mtinge 'Bartez' sijawahi kuamini kama ameshuka kiwango zaidi ya siasa za Simba na Yanga.
Akiwa katika ubora wake jana alifungwa goli moja katika dakika 29 na Walter Musona akimalizia pasi ya Donald Ngoma aliyempiga chenga beki Juma Abdul upande wa kulia wa uwanja.
Mapema dakika ya 12, Bartez alionyesha maajabu baad aya kuokoa kwa mguu shuti la 'hapa na hapa' la Donald Ngoma na mpira ukamkuta Tathit Kamusoko aliyepigwa nje.
Hakika alitukuka kwa kiwango chake na kila Mwanayanga alikunwa na kiwango chake.
Bartez alikaa sawa goli, alikaa nafasi sahihi wakati wote na akili yote ilikuwa mchezo kwasababu yuko huru na ameaminiwa na kocha.
Baada ya mechi kumalizika katika mitandao ya kijamii, watu wengi wa Yanga waliandika jina la Ally Mustapha Mtinge 'Bartez' wakifurahishwa na kiwango chake nikiwemo mimi.
Lakini haya yametokana na weledi wa viongozi wa Yanga waliouonesha baada ya kufungwa 1-0 na Simba. Hawakuonekana kupaniki kama walivyofanya baadhi ya mashabiki wasiokosa lawama.
Shabiki kulaumu ni haki yake, yeye hataki kufungwa siku zote na anaogopa kuchekwa hususani na mtani, lakini mpira una makosa ya kawaida kama alivyofanya Bartez. Makipa wengi wazuri wanafungwa magoli ya kizembe kuliko la Bartez. Unakumbuka fainali za kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana? unadhani Iker Casillas wa Hispania angecheza tena mpira kama ingekuwa Bongo kwa namna alivyoiuza Hispania kwa makosa binafs?
Lakini Wahispania wote walikaa upande wake, kocha Vicente del Bosque akaendelea kumuweka kipa namba moja na anaendelea kudunda Real Madrid na timu ya Taifa.
Nilihofia kumpoteza tena Bartez baada ya mechi ya Simba, niliingiwa na hofu kwani nilidhani atatolewa Kafara. Namheshimu sana Pluijm, hana mpango na maneno ya mtu, anaamini kwenye kukosea katika mpira. Ameendele kumuamini Bartez kama kawaida.
Viongozi wa Yanga naona safari hii hawakuwa 'wajinga'. Walituliza akili zaidi.
Kutokana na Yanga kufuta ujinga baad aya kufungwa na Yanga kumeleta matunda ya Bartez jana.
Hongera sana Bartez, endelea kukaza wazidi kukuelewa.
Pia naamini Dida atarudi kwani bado ni kipa mzuri. Sema kwenye mpira ni nafasi tu. Hata ulaya kuna kipa namba moja na mbili. Lakini naamini Dida anaweza kuwa namba moja na Bartez pia. Wakabadilishana.

Maoni: 0712461976

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video