Msuva (kushoto) na Danny Mrwanda ni watu hatari Yanga
Na Mwandishi Wetu
HAWAKUWA na muda wa kupoteza baada ya kukamilisha kazi iliyowapeleka Zimbabwe jana wakiitoa Platinum kwa wastani wa mabao 5-2 katika mechi mbili za raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga wamewasili Dar es salaam usiku wa kuamkia leo kwa ndege maalumu ya serikali na kuanza maandalizi ya mechi ya jumatano (aprili 8 mwaka huu) dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Ikiwa na mafanikio ya kutinga hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho wana nafasi kubwa ya kuifunga Coastal Union ambayo ameendele kusuasua.
Jana kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, Coastal chini kocha Jamhuri Kwhelo walipigwa 1-0 na vibonde Prisons na kuwachukiza mashabiki wake kwa kiasi kikubwa.
Mashabiki hao walitukana 'mitusi mizito' ambayo siwezi kuandika hapa kwasababu za kimaadili.
Coastal wakiwa na msongo wa mawazo wanakwenda kukabiliana na Yanga iliyobora na amani imetawala.
Kumbuka wanaongoza ligi kwa pointi 40 baada ya kucheza mechi 19 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 36 baada ya kucheza mechi 18.
Msuva weka mbali na watoto msimu huu
Siku Yanga wanachuana na Coastal Union, Azam fc watakuwa kibaruani dhidi ya Mbeya City ambayo jana ilitoka sare ya 1-1 na Ndanda fc uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara.
Kwa kiwango walichoonesha Yanga jana, muunganiko wa kiungo na ulinzi na safu ya ushambuliaji, wanaonekana kuwa na asilimia kubwa ya kushinda mechi ijayo dhidi ya Coastal Union.
Kwa siku za karibuni Yanga imeimarika safu zote. Jana Haruna Niyonzima, Nadir Haroub 'Cannavaro' Kelvin Yondani na nyota wa mchezo Ally Mustapha Bartez walionesha ubora mkubwa na kwa namna hiyo Coastal wajiandae vizuri.
Kumbuka Yanga ndiyo timu pekee iliyofungwa mabao machache mpaka sasa (magoli 11) ikifuatiwa na Azam fc waliofungwa magoli 12.
Pia wanaongoza kwa kufunga magoli mengi (mabao 28) wakifuatiwa na Azam fc magoli 25. Kwa maana hii, Yanga ndiyo timu yenye safu bora ya ulinzi na ushambuliaji kwa sasa ligi kuu.
Wanaingia wakiwa uwanjani wakiwa wanaongoza kwa kila kitu katika msimamo (pointi, magoli mengi ya kufunga na kufungwa machache), hivyo hii inawapa morali kubwa zaidi ya kuichapa Coastal ingawa lolote linaweza kutokea.
Pia Yanga wana mshambuliaji anayeongoza kwa magoli mengi katika orodha ya wafungaji, Simon Msuva (Magoli 11) akifuatiwa na Didier Kavumbagu magoli 10 na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar magoli 9.
Sio kwamba Coastal wabaya, hapana, lakini kiufundi lazima uangalia nani yuko sawasawa zaidi ya mwenzake, kwasasa Yanga ni bora zaidi ya Coastal.

0 comments:
Post a Comment