Tuesday, April 7, 2015

Katika kikosi kinachoonekana pichani wachezaji wanne

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefikisha pointi 35 katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara, pointi moja nyuma ya Azam fc waliopo nafasi ya pili, lakini Wanalambalamba wana mechi 3 zaidi mkononi.
Mechi ya jana ilikuwa ya 21 kwa Simba, na katika mechi sita zilizosalia kabla ya jana, Mnyama ana hesabu ya kuvuna pointi zote 18 na jana wameanza kwa kuwachapa Kagera Sugar.
Sasa Simba wamebakiza pointi 15 katika mechi 5 zilizosalia.
Mashabiki wa Simba walishangaa kuona wachezaji 7 wa kikosi cha kwanza wa Simba hawapo ingawa wengine wanaanzia benchi.
Maswali mengi yaliibuka, wako wapi wengine?
Kocha wa Simba Goran Kopunovic alikuwa na hofu ya kuwakosa wachezaji muhimu, lakini alikaa chini na kuwapanga kisaikolojia vijana wake kwamba anawaamini na watapata ushindi.
Kweli jana wakafanya mambo kwa kuifunga Kagera Sugar 2-1 uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga;
Wachezaji sababu wa Simba waliokosekana jana na sababu zao;
1. JUUKO MURSHEED: Yupo kwao Uganda akidaiwa kuwa na matatizo ya kifamilia, lakini taarifa za ndani zinadai kuna fedha hajalipwa na uongozi wa Simba kama matakwa ya mkataba wake yanavyosema.

2. SIMON SSERUNKUMA: Naye yuko kwao Uganda kwa sababu kama za Mursheed.

3. ABDI HASSAN BANDA: Anauguliwa na mama yake, hivyo ameungana na familia yake kumuuguza. Hayupo kabisa katika kambi ya Simba.

4. ELIAS MAGULI: Jana hakucheza kabisa licha ya kuwepo katika wachezaji wa akiba, sababu ni kwamba aliomba ruhusa kwenda kwao Mara kuwaona wazazi wake, lakini alirudi akiwa amechelewa, hivyo akaondolewa katika kikosi kilichoaanza.

5. JONAS MKUDE: Aliondoka kambini na kurudi Dar es salaam baada ya kufiwa na baba yake mwishoni mwa wiki .

6. IVO MAPUNDA: Alikosekana kwasababu anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mechi dhidi ya Mgambo JKT. Mechi ya jana ni ya pili kuikosa, kwani aliikosa ya Ruvu Shootings ambayo Simba walishinda 3-0 uwanja wa Taifa.

7. HASSAN KESSY: Ametofautiana na viongozi wa Simba akidai fedha zake za usajili zilizobakia kulipwa na anataka kutimiziwa mambo alivyoahidiwa na uongozi wa Simba wakati anasajiliwa likiwemo nyumba na gari.


0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video