Tuesday, April 7, 2015

Wanachama wa tawi maarufu la Mpira na Maandeleo la jijini Dar es salaam 'Simba Ukawa' walipata ajali ijumaa jioni mkoani Morogoro wakielekea mkoani Shinyanga

SIMBA SC jana ikiwa ugenini ilishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Magoli ya Simba yalifungwa na Ramadhani Singano na Ibrahim Hajibu aliyefungwa kwa penalti.
Bao la Kagera lilifungwa na Rashid Mandawa ambaye amefikisha idadi ya mabao 10 msimu huu.
Baada ya mechi hiyo, mtandao huu ulifanya mahojiano na nahodha wa Simba, Hassan Isihaka ambaye alifunguka;

"Wachezaji wengi muhimu hawapo kikosini kwasababu mbalimbali, hakika tulikuwa na wakati mgumu, tulifanya vikao vingi na kocha akitueleza nini cha kufanya. Tuna majanga acha kabisa, mashabiki wetu 7 wamefariki katika ajali, inaumiza sana, tukakaa chini na kuona tuna deni la kuwaondolea huzuni japo kidogo wanasimba. Ajali hii imetufanya tuwe wanyonge na ikatufanya tuongeze nguvu mara mbili zaidi ili kuwaondolea majonzi Wanasimba" Alisema Isihaka na kuonegeza: "Baadhi ya wenzetu wana matatizo ya kifamilia, Mkude kafiwa na baba yake, angesikia tumefungwa ingemuuma zaidi".
"Viwanja vya mikoani ni vigumu kucheza, leo (jana) ukiangalia uwanja wa Kambarage haukuwa katika hali nzuri kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, lakini tumepambana na kupata pointi tatu mbele ya Kagera Sugar".
"Hawa jamaa (Kagera) ni wagumu haswa! wamecheza vizuri, lakini tulishirikiana kuhakikisha hawapati matokeo kama mwaka jana". Aliongeza Isihaka.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video