Kifo cha Marsh kiliwaumiza wadau wengi wa soka, lakini kazi ya Mola haina makosa. Mwenye enzi Mungu aendelee kulaza mahaka pema peponi roho ya Marehemu. Amina
Na Kassim Mtolea, Mwanza
KAMA unakumbuka wimbo wa msondo ngoma "tunatoana roho yarab kwa mali alizoacha baba"ndicho kilichopo kwa familia ya marehemu Sylvester Marsh.
Familia ya kocha huyo msaidiz wa Taifa Stars imesema haitaki kituo chake cha soka kuendelea kutumia jina la marehemu.
Hayo yamenenwa na familia ya kocha huyo iliyopo maeneo ya Igoma walipotembelewa na MPENJA BLOG.
Mwanahabari alifika hapo baada ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa matumizi mabaya ya pesa za rambirambi kwa watu waliokuwa karibu na Sylvester Marsh.
Kaka mkubwa wa marehemu, Merickyor Marsh alisema wamefikia maamuzi hayo kutokana na baadhi ya watu kutumia kituo hicho kujipatia fedha kupitia rambirambi zinazotolewa na wadau wa soka.
Kituo cha Marsh Academy kipo katika kata ya Milongo hapa jijini Mwanza, baada ya kifo cha Marsh kituo hicho sasa kinaongozwa na Hamad Ally ambaye alikuwa mtu wa karibu wa marehemu Sylvester Marsh.


0 comments:
Post a Comment