KOCHA mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm hataki kushindwa kitu na akipanga jambo lake anapenda kuona linatimia.
Uongozi wa Yanga ulituma taarifa CAF kwamba mchezo wao wa kesho dhidi ya Etoile du Sahel utaanza saa 9:00 alasiri badala ya saa 10:00 muda uliozoeleka kwa vijana wa Jangwani.
Lengo la viongozi lilikuwa kuwachezesha Etoile wakati wa jua kali na kuwaathiri, lakini Pluijm aligoma kabisa akieleza kuwa muda huo unaweza kuwaathiri vijana wake pia na anataka mechi ichezwe saa 10:00.
Mashindano ya Africa hayana uswahili na huwezi kubadili muda kienyeji na ndipo uongozi wa Yanga ukaanza kuhangaika kubadili muda kupeleka saa 10:00 kwa matakwa ya Pluijm.
Mpaja jioni bado CAF walikuwa hawajatoa jibu, lakini sasa wameshaijibu Yanga rasmi kuwa mchezo huo wameruhusiwa kuanza saa 10:00 jioni jioni.
Yanga na Etoile zinachuana katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho na mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili zijazo.


0 comments:
Post a Comment