KAGERA SUGAR FC tayari wametua mkoani Mtwara kujiwinda na
mechi ya kesho kutwa dhidi ya wenyeji wao Ndanda fc itayopigwa uwanja wa
Nangwanda Sijaona.
Wakata miwa hao wanashika nafasi ya tano katika msimamo wa
ligi kuu wakijikusanyia pointi 31 baada ya kucheza mechi 24, sawa na Mbeya City
waliopo nafasi ya nne kwa pointi 31 pia, lakini wana wastani mzuri wa magoli ya
kufunga na kufungwa.
Kagera Sugar wamefunga magoli 22 na kufungwa 24, tofautiya
magoli ni -2 wakati Mbeya City wao wamefunga magoli 21 na kufungwa 21, hivyo
tofauti ni 0.
Kocha msaidizi wa Kagera Suagr, Murage Kabange amesema mechi
ya kesho kutwa ni ngumu kutokana na Ndanda kuwa katika hatari ya kushuka
daraja, lakini wamejipanga kupata ushindi.
“Mechi ya keshokutwa ni fainali kwa Ndanda, tunalijua hilo
na ukizingatia tuko nyumbani kwao, lakini kwa kiasi fulani tumejitayarisha
kukabiliana nao ili kuhakikisha tunapata matokeo”. Amesema Kabange na kuongeza:
“Kama unavyojua mpira ni mchezo wa makosa na daima una mambo matatu, kushinda,
kufungwa na kutoa sare, mojawapo lazima litokea, lakini lengo letu ni kupata
ushindi na yanayobaki tunamuachia Mungu. Kikosi kipo vizuri na tunachosubiri ni
mechi tu”
0 comments:
Post a Comment