Friday, April 10, 2015

Na Augustino Mabalwe,Dar es salaam
Mshambuliaji wa klabu ya Psg Zlatan Ibrahimovic amefungiwa mechi 4 huko katika ligi ya Ufaransa kwa kosa la kuponda uendeshwaji wa ligi hiyo.
Tukio hilo lilitokea baada ya Psg kupokea kipigo cha 3-2 kutoka kwa Bordeaux mwezi uliopita ambapo msweden huyo alinaswa na kamera akizungumza lugha chafu juu ya waamuzi wa mechi hiyo na huku akiitusi nchi hiyo kwa madai ya kushindwa kuendesha soka.
Hata hivyo Ibrahimovic aliomba msamaha baada ya kufanya hivyo lakini chama cha cha soka nchini humo kimeamua kimfungie ili iwe fundisho.
Kutokana na adhabu hiyo ,sasa Zlatan atakosa mechi za ligi dhidi ya Nice,Lille,Metz na Nantes
Hili ni pigo kubwa kwa klabu ya Psg kumkosa mshambuliaji huyo ambaye alifunga hat trick katika mechi ya juzi dhidi ya St Etienne katika kombe la Coup de France.
Psg ipo kileleni mwa ligi kuu nchini Ufaransa kwa tofauti ya pointi 1 na wanaoshika nafasi ya pili Lyon,huku wakiwa wamebakisha mechi 7 kumaliza ligi hiyo msimu huu.
Aidha Zlatan Ibrahimovic,33, atakosa mechi ya kwanza ya robo fainali ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Barcelona wiki ijayo kufuatia kadi nyekundu aliyoipata katika mechi ya pili ya hatua 16 bora dhidi ya Chelsea

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video