Thursday, April 16, 2015

Kocha Jurgen Klopp alivyotangaza kwamba ataihama timu yake ya Borussia Dortmund imekua story kubwa wiki siku ya leo. Kila mwandishi amejaribu kuandika kitu chake lakini hizi ndizo sababu tano ambazo ndizo zinaweza kuwa ni sababu kubwa kwa Klopp kutaka kuihama Borussia Dortmund.
1.Kuondoka kwa Gotze
March 27 Mario Gotze alisaini mkataba na Borussia Dortmund hadi mwaka 2016 lakini mkataba wake ulikua na kipengele cha kumruhusu kuhama lakini na ada angalau isiyopungua €37 million. April 23 mwaka 2013 ilitangazwa Gotze anasepa kwenda kwa wapinzani waoBayern Munich baada ya kupangua hicho kipengele cha ada ya €37 million. Klopp alikubali kwamba hajafurahia muda wa kuondoka kwa Gotze kwasababu ilikua ni masaa 36 kabla ya mechi yao ya nusu fainali na Real Madrid kwenye UEFA. Baadae Klopp alisema Dortmund haikua na nafasi ya kumshawishi Gotze.
Wakati Gotze ana hama alikua ni mmoja ya tegemeo ukizingatia alikua ni zao ya academy ya Borussia Dortmund.
12
2. Kuondoka kwa Lewandowski
Baada ya Gotze kusepa Borussia Dortmund ikaingia movie mpya ya Robert Lewandowski ambapo Borussia ilikamia kutokumuuza kwasababu thamani yake ilikua kubwa sana akiwa kwenye hiyo club. Mwisho wa siku mambo yakawa kama ya Gotze na yeye akahamia kwa wapinzani wa Munich.
3.Kufeli kwa Plan B

Soka ni biashara inayoenda kwa haraka sana, wachezaji wadogo wakati Klopp anawika na Borussia walikua wana unauwezo mkubwa wa kucheza na kupeana pasi nzuri, kupeana nafasi na hadi kutafuta nafasi.Mara ya mwisho Dortmund imecheza mchezo huu ilikua ni mechi ya kwanza ya msimu wa Champions League na Arsenal. Klopp aliona/alipata matatizo haya lakini plan B yake haijafanikiwa.
4. Hakuna damu mpya kwenye timu
Borussia Dortmund walikua na kikosi kilichokua kinatisha ujerumani au hata Ulaya. Team nzima ilikua na vijana wadogo wenye njaa na nguvu, pia wote hawana mataji, hawana mafanikio makubwa.Kwa hiyo walikua na njaa ya kutafuta mafanikio kwa nguvu zote. Tofauti na sasa baada ya wote kuchukuliwa na timu kubwa.
5. Klopp amekua mkubwa zaidi ya Borussia
Kama ilivyokua kwa Arsene Wenger na Arsenal au Sir Alex Ferguson kwa Manchester ndivyo ilivyokua kwa Klopp akiwa Borussia japokuwa yeye hakutaka ijulikane hivyo bado aliendelea kuipenda club na kusisitiza club ni kubwa zaidi yetu wote.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video