SIMBA SC imetamba kumaliza hasira zake kwa Mgambo
JKT katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara watakayokutana keshokutwa uwanja wa
Taifa Dar es salaam.
Afisa habari wa Simba, Hajji Sunday Manara
alikaririwa na mtandao huu jana akikiri kuzidiwa na Mbeya City mechi iliyopita
uwanja wa Sokoine na kufungwa 2-0, lakini akadai Mgambo waje vizuri kwani
watamaliza hasira zao kwao.
Baada ya kusikia maneno hayo, kocha mkuu wa Mgambo
JKT, Bakari Shime amejibu mapigo akisema walichokifanya Mkwakwani watakirudia
tena uwanja wa Taifa.

“Walipokuja kwetu tuliwafunga 2-0, nilisema
ukiangalia wachezaji wa Simba na Mgambo, sisi tuna uzoefu kuliko wao. Angalia
mtoto kama Banda (Hassan) nimemfundisha mwenyewe, akina Mkude (Jonas), Ndemla
(Said) nilikuwa nawafunga tu katika michuano ya vijana” Amesema Shime na
kuongeza: “Kwa wachezaji kama hawa nitawaogopa? Mimi sijali Simba wala Yanga,
naingia kutafuta pointi tatu, tutaonana uwanjani jumatano”.


0 comments:
Post a Comment