Friday, April 17, 2015


MLINZI wa kati wa Azam fc, Said Hussein Morad ametangaza kuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Katika mahojiano maalumu na mtandao huu, Morad amesema mkataba wake umemalizika jana aprili 16 mwaka huu na Azam hawajaonesha nia ya kumuongezea mkataba mpya.

“Namshkuru Mungu nimeishi na Azam vizuri, hakuna matatizo yoyote yaliyotokea na hata kama mashabiki wanadhani kuna matatizo yametokea, kwangu mimi hakuna matatizo na hivi sasa mimi ni mchezaji huru, amesema Morad na kuongeza: “ Mkataba wangu umeisha na ndio maana mashabiki wangu hawanioni kwenye timu.

“Mkataba wangu umeisha jana tarehe 16/4/2015. Sijawahi kukaa na viongozi ila taarifa nilifikisha mpaka kwa meneja na yeye akafikisha mpaka kwa kocha, lakini baada ya hapo hawanielezi chochote”. Amesema Morad.

VIPI KUHUSU TAARIFA ZA KUFUNGIWA MECHI 4 PAMOJA NA AGGREY MORRIS NA KIPRE TCHETCHE?

Morad amejibu: “Mimi nilikuwa sijasimamishwa, niliomba ruhusa, katika msiba wa Simba Ukawa kulikuwa na familia yangu, wale Marehemu mmojawapo ni damu yangu (mjomba wake Rajab Uhadi Mtoro), Azam walinipa ruksa ya siku mbili, lakini maiti kutoka Morogoro ikachelewa kuja Muhimbili, ilikuja kama saa 11 alfajiri na kufanya michakato ya pale ilichukua muda na unajua Muhimbili maiti haiwezi kutoka mpaka kuandikisha jina. Nikawa nasubiriwa mimi kwasababu ndiye niliyeandikisha jina na baada ya kufika ndipo michakato ikaanza”.

“Tukaanza kuosha maiti na kusafirisha mpaka Bagamoyo nyumbani na baadaye tukafikisha kijijini kwetu Kigogo na kuzika”

KURUDI KAMBINI ILIKUWAJE SASA?

Morad anasema: “Siku ya pili ilitakiwa niripoti kwenye mechi, tulikuwa tunacheza na Mbeya City na mini nikawa njiani kurudi na nilipofika nikarudi na kwenda moja kwa moja kambini siku ya mechi”.

AKAAMBIWA NINI?

Morad anatiririka: “Baada ya mechi kuisha,  jioni nikaambiwa Morad inabidi urudi nyumbani mpaka tutakapokwenda Morogoro na Tanga, tukirudi kutoka Tanga tutakuita, kocha ananiambia kitu kama hicho”

“Baada ya pale nikamwambia kocha mimi mkataba wangu unaishi mpaka siku hiyo na nitakuwa nimeshamaliza mkataba na Azam”

ILIKUWAJE AKAHUSISHWA NA UTORO WA KIPRE, MORRIS?

Morad anafafanua: “Aggrey Morris, Kipre Tchetche walisimamishwa kwa matatizo yao na namimi nikachanganywa,mimi niliwaomba ruksa, sema baada ya kuwaomba hiyo ruksa nilipoenda kambini nikajumuishwa kundi la akina Aggrey, lakini mimi sina kosa lolote”

“Hapo kwenye kujumuishwa sijui kwanini ilikuwa hivyo, ujue kila mtu na maisha yake, kama kocha ana mapungufu yake au mchezaji nina mapungufu yangu,  lazima  uongozi ukae na kuamua”

IMEKUWAJE AMEWAAMBIA AZAM FC KWA MUDA MREFU KUHUSU KUONGEZA MKATABA LAKINI WAMEMCHUNIA?

Morad anasema: “Naamini hawanihitaji kwasababu niliwaambia muda mrefu kabla miezi miwili haijaisha”

VIONGOZI WA AZAM WALIMFARIJI MSIBANI?

Morad anasisitiza: “Hakuna hata kiongozi mmoja wa Azam aliyekuja kwenye msiba wangu isipokuwa wa Simba waliowafuata watu wao

.Wachezaji walionipigia simu ni Aggrey na Mwaikimba na Erasto”.

VIPI MIPANGO YAKE?


Morad anasema: “Kama timu yangu ya Azam itaniongeza mkataba nitafanya kazi kwasababu sina kinyongo na timu yoyote Tanzania. Kama hawataniongeza nipo tayari kuichezea timu yoyote”.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video