UONGOZI wa Azam fc umewarejesha kambini
wachezaji wake wawili kabla ya kumaliza adhabu waliyopewa ya kufungiwa mechi
nne kwa kosa la kuondoka kambini bila kuaga.
Kipre Tchetche na Aggrey Morris walifungiwa
mechi nne kuanzia ile ya sare ya 1-1 na Mbeya City, 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar
na 0-0 na Mgambo JKT, lakini wamerejeshwa kuelekea mechi ya nne katika kifungo
chao dhidi ya Kagera Sugar hapo kesho uwanja wa Azam Complex.
Azam wanashika nafasi ya pili kwa
kujikusanyia pointi 39 katika mechi 21 walizocheza, pointi saba nyuma ya vinara
Yanga waliocheza mechi 21 pia.
Katika sare tatu walizopata mfululizo,
safu ya ulinzi ilicheza hovyo baada ya kumkosa Aggrey Morris ambaye anacheza
vizuri na Paschal Wawa, lakini safu ya ushambuliaji pia iliyumba kwasababu
Didier Kavumbagu alikosa mtu sahihi ambaye ni Kipre Tchetche.
Mechi dhidi ya Mgambo, Kavumbagu
alicheza na Gaudence Mwaikimba ambaye dhahiri ameshaisha kiuchezaji kwasabbau
ya umri na kutopangwa kabisa msimu huu.
Naye Wawa alicheza na Mwantika dhidi ya
Mbeya City na Mtibwa Sugar, lakini waliyumba kwasababu hayuko imara.
Uongozi wa Azam ulitangaza kuwa Kipre
na Morris ni majeruhi wakati sio na mtandao huu ukawashauri kuwaponya kiaina na
kuwarudisha kambini na imekuwa hivyo.
Muda huu vijana hao wapo kambini
Chamazi wakiwasubiri Kagera Sugar kesho ambayo hawakustahili kucheza kama uongozi ungeendelea kushikilia msimamo wake.

.jpg)
0 comments:
Post a Comment