Takwimu zilizotolewa na maafisa wa mchezo wa kiungwana wa FA
zinaeleza kuwa Chelsea ni timu inayoongoza kutoheshimu maamuzi ya waamuzi katika
ligi kuu England, huku makocha wa timu hiyo wakishika nafasi ya pili kwa utovu
wa nidhamu wakati wa mechi.
Liverpool imetajwa kuwa klabu yenye heshimu kubwa kwa
waamuzi katika kipengele hicho
kilichobeba alama saba ikifuatiwa na Burnley na West Brom.
Klabu za Arsenal na Stoke City zipo katikati katika orodha
hiyo ambapo kanuni zinaeleza kuwa kitendo cha kuheshimu maamuzi yenye utata
bila kugoma au kumzonga muamuzi kinaipa timu alama saba wakati tabia ya
kukubali maamuzi halafu kuonesha ishara za kutoheshimu zinatolewa alama sita.
FA wanatoa alama kwa kuangalia maeneo sita ambayo ni kadi
nyekundu na njano, mchezo mzuri, heshima kwa wapinzani, heshima kwa waamuzi,
tabia ya maafisa wa timu na mashabiki.
Alama kumi zinatolewa kwa kadi nyekundu ambapo timu inapunguziwa
alama moja kwa kadi ya njano na alama tatu kwa kadi nyekundu.
Mchezo mzuri una alama kumi zinazotolewa kwa kucheza soka la
kuvutia, kushambulia sana na kushinda, lakini timu ikitumia mbinu za kujilinda
na udanganyifu alama zinapunguzwa.
Alama saba zinatolewa katika kipengele cha heshima kwa
wapinzani kinachohusisha kuwaheshimu wachezaji pinzani na kuonesha mchezo wa
kiungwana, wakati alama saba pia zinatolewa kwa kuheshimu waamuzi na maafisa wa mechi.
Alama sita zinatolewa kwa maafisa wa timu wakiwemo makocha
dhidi ya waamuzi, wakati alama kumi
zinatolewa kwa tabia ya mashabiki ambapo alama zote zinatolewa kwa
mashabiki wanaokubali matokeo, wakati wakitumia lugha ya matusi kwa wachezaji, waamuzi na
kuwatishia mashabiki pinzani alama zinapounguzwa.


0 comments:
Post a Comment