Wednesday, April 15, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Yanga na Etoile zote ziliwahi kumsajili kiungo wa kimataifa wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Anord Okwi kwa nyakati tofauti na kuzisababishia hasara ya mamilioni ya shilingi.'
WAMESHTUKA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya wapinzani wa Yanga SC katika michuano ya kimataifa kwa sasa, klabu ya Etoile Sportive du Sahel (ESS) kupangua tarehe ya kuwasili Tanzania.
ESS, vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ya Tunisia kwa sasa wakiwa na pointi 50 baada ya mechi 23, wamepangwa kukutana na Yanga SC katika hatua ya 16 ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.
Awali mabingwa hao wa zamani wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika, walitoa taarifa kwamba wangetua jijini Dar es Salaam leo Jumatano, lakini wamepangua ratiba hiyo.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro, ameuambia mtandao huu kuwa wageni wao wamewataarifu kuhusu mabadiliko ya kutua kwao nchini.
"Leo nilipoamka tu alfajiri nimeona email kutoka Etoile du Sahel ambayo inasema watakuja nchini saa 8 usiku kwa saa za Tunisia siku ya taerehe 17 mwezi huu," amesema Muro huku akiweka wazi kwamba wageni wao hao hawajaeleza sababu za kupangua kwa ratiba ya ujio wao nchini.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video