KATIKA kile kinachoonekana wamepania kufanya kweli kimataifa,
uongozi wa Yanga umewaahidi wachezaji wake mamilioni ya fedha ikiwa ni
zawadi endapo ikiing'oa Etoile Sportive du Sahel (ESS) ya Tunisia katika
michuano ya kimataifa mwaka huu.
Yanga, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, wamepangwa kuchuana dhidi ya ESS katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika wakianzia nyumbani jijini Dar es Salaam Jumamosi kabla ya kurudiana mjini Tunis, Tunisia kati ya Mei 1-3, mwaka huu.
Ili kuhakikisha ESS haisongi mbele, uongozi wa Yanga jana ulifanya kikao kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo zilizopo makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga jijini na kudai kukubaliana kuandaa kiasi cha Sh. milioni 500 kama motisha kwa wachezaji endapo wataing'oa Etoile.
"Leo tumekuwa na vikao vizito vya uongozi hapa klabu (jana). Kikubwa tumekubaliana kutoa zawadi ya Sh. milioni 500 ambazo zitakuwa zawadi kwa timu endapo itafanikiwa kuing'oa Etoile du Sahel," NIPASHE lilidokezwa na mmoja wa viongozi wa Yanga aliyeshiriki katika kikao hicho.
Kiongozi huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa klabu, aliendelea kueleza kuwa wamepanga mikakati mingine mingi ambayo wanaamini itaisaidia timu yao kuwang'oa mabingwa wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2007 na Kombe la Shirikisho barani 2006.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, alisema kikosi chao kimeweka kambi katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam kuwanolea makali ESS.
Muro alisema kiungo wao Salum Telela aliyekanyagwa miguuni na mshambuliaji Themi Felix wa Mbeya City katika mechi yao ya juzi, anatarajiwa kufanya mazoezi mepesi leo ingawa afya yake bado haijaimarika.
Yanga imetinga katika hatua hiyo baada ya kuzing'oa BDF XI FC ya Botswana (mabao 3-2) na FC Platinum ya Zimbabwe (mabao 5-2).
Etoile kutua nchini kesho
Wakati huo huo Muro aliliambia gazeti hili jana kuwa wapinzani wao, Etoile du Sahel wanatarajiwa kuwasili nchini kesho mchana kwa ajili ya mechi yao itakayopigwa Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni chini ya waamuzi kutoka Msumbiji.
Alisema msafara wa Waarabu hao wa Tunisia utatua jijini ukiwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi 10.
Muro alisema wageni hao wamekataa kusema watatua kwa usafiri wa ndege gani lakini katika taarifa yao ya awali walieleza bila kutaja pia majina ya wachezaji.
"Timu yetu imeshaingia kambini na leo (jana jioni) itaanza kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ambao utatumika Jumamosi," alisema Muro.
Aliongeza kwamba uongozi wa Yanga unaendelea na mipango yake kuhakikisha timu yao inafanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.
"Tunataka kufanya vizuri hapa nyumbani kabla ya kwenda ugenini, tunajua umuhimu wa ushindi wa nyumbani na mwaka huu tumejipanga kuweka rekodi ya kuwaondoa Waarabu", aliongeza kiongozi huyo.

CHANZO: IPP MEDIA.

0 comments:
Post a Comment