Monday, April 13, 2015


COASTAL Union ikitoka kupigwa 8-0 jumatano ya wiki iliyopita dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa ilishinda 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyochezwa uwanja wa Azam Complex jumamosi ya juma lililopita.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa, kuna tukio moja lilitokea likimhusisha mlinda mlango wa Coastal Union, Shaban Hassan Kado na mchezaji mmoja wa JKT Ruvu ambaye Kado amedai hamkumbuki kwa jina.
Kado alipigwa na njuma sehemu ya mbavu na kuumizwa na mwanajeshi huyo baada ya kudaka mpira kwa kuulalia kufuatia shuti lililogonga mwamba na kurudi chini.
Kado amezungumza na mtandao huu mchana huu na kueleza kisa hicho;

"Niliumia kwenye mechi ya JKT Ruvu jumamosi, kwa bahati mbaya kuna mshikaji simkumbuki jina lake alinikanyaga.

ILIKUWAJE AKAPIGWA TEKE HILO?

Kado anasema: "Si unajua purukushani za langoni, lilipigwa shuti likagonga mwamba na mpira kurudi chini, wakati jamaa anakuja kumalizia mimi nikaulalia na wakati anajaribu kupiga mpira akanipiga kwenye mbavu"

HALI YAKE KWA SASA INAENDELEAJE?

Kado anajibu: "Nashukuru Mungu naendelea 'fresh' , maamivu yalikuwa makali lakini sikuumia kwa ndani, nimepata dawa na ninaendelea safi"

VIPI KUHUSU MAZOEZI NA ATARUDI LINI KAMBINI TANGA?

Kado anaeleza: "Niko fresh na leo asubuhi nimeanza mazoezi hapa nyumbani kimara. Kambini nitaripoti jumatano Tanga".

Kado ni miongoni mwa makipa wakubwa nchini, lakini mara kadhaa amekuwa akikaa benchi katika timu yake ya Coastal Union, mfano siku waliyolala 8-0, kipa kijana Fikirini Bakari alisimama langoni.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video