Monday, April 13, 2015

Timu ya Mtwivila  city ya mjini Iringa ipo kwenye maandalizi makubwa kujiandaa na michezo ya kumtafuta bingwa wa mikoa ili iweze kupanda ligi daraja la pili
Katika kuhakikisha inafanya vizuri timu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Mtwivila hapa  Iringa  mjini, kwa sasa inafanya  mazoezi yake katika viwanja vya chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa ambapo lengo kubwa la timu hiyo ni kupanda daraja msimu wa 2015-2016 utakaoanza baadaye mwaka huu.

Pamoja na hayo lakini bado timu hiyo ya Mtwivila city ina ukata wa fedha na sasa wapenzi na wadau wa soka wanaombwa kuichangia kwa hali na mali ili iweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ya ligi ya mabingwa wa mikoa inayotazamiwa kuanza kutimua vumbi karibuni

Makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Ibrahim Tungo alisema

 ‘‘Naomba sana wadau na wapenzi wa soka mkoa wa Iringa  watusaidie katika  mapambano yaliyo mbele yetu kwani tunatakiwa kushiriki kikamilifu na hata tupande daraja pamoja, mafanikio ya Mtwivila city ni mafanikio ya soka la Iringa tukiungana pamoja tutaweza kukidhi azma yetu ’’


Pamoja na hayo,  timu hiyo ambayo kwa sasa ni gumzo kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa  imepata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la MUUNGANO LA MUFINDI ambalo linatazamiwa kuanza kutimua vumbi katika wilaya ya MUFINDI mapema mwezi wa tano .


Timu ya Mtwivila city yenye wachezaji wengi ambao bado wapo masomoni inatazamiwa kutoa ushindani mkali katika  michuano ambayo itashiriki .

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video