UTAMPENDA tu Luis Suarez! ametupia mawili Barcelona ikiIbuka na ushindi ugenini wa mabao 3-0 dhidi ya Paris Saint Germain (PSG) katika mechi ya kwanza ya ligi ya mabingwa iliyomalizika usiku uwanja wa Parc des Princes, Mjini Paris, Ufaransa.
Suarez amefunga magoli yake katika dakika ya 67' na 79' akipata pasi zote kwa Javier Mascherano.
Mapema dakika ya 18', kijana mwenye kipaji kikubwa cha soka, Mbrazil, Neymar Jr amefunga goli la kuongoza kwa Barcelona akipata pande kutoka kwa Lionel Messi.
Goli la PSG limefungwa na Greygory van der Wiel katika dakika ya 82'.
Takwimu za mechi hiyo zinaonesha kuwa Barcelona walipiga mashuti 5 yaliyolenga lango na matatu wamefunga, wakati PSG wamepiga matano pia na moja tu ndio limetikisa nyavu.
Barcelona wazee wa Burudani kama kawaida yao wamemiliki mpira kwa asilimia 61 kwa 31 za PSG.
Kwa matokeo hayo, Barcelona wamekaa mguu nje ndani kwasababu watahitaji sare yoyote ile Camp Nou au kufungwa 1-0 au ushindi ili kutinga hatua ya nusu fainali.

0 comments:
Post a Comment