Quaresma alikuwa moto mkali leo
Bayern Munich hawatamsahau Ricardo Quaresma mwaka huu kwa kile alichowafanyia katika uwanja wa Estadio do Dragao, Ureno usiku huu!.
Jamaa ndani ya dakika 10' amewaadhibu mara mbili katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Quaresma amefunga goli la kwanza dakika ya 4' tu kwa mkwaju wa penalti na katika dakika ya 10' akapiga msumari wa pili.
Dakika ya 28' Thiago Alcantara aliwasawazishia goli la kwanza Bayern Munich, lakini mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika, Porto walikuwa mbele kwa magoli 2-1.
Kipindi cha pili, Wareno waliendelea kulisakama lango la Bayern na katika dakika ya 65' Jackson Martinez aliandika bao la tatu na la mwisho leo.
Bayern wanahitaji kufanya kazi kubwa katika mechi ya marudiano kwenye uwanja wao wa Allianz Arena jumanne ya wiki ijayo.
Bayern wanahitaji ushindi wa magoli 2-0 ili kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini au wapate ushindi wa 3-0 kwa kusonga mbele bila kanuni.
Porto wanahitaji sare au kufungwa 1-0 katika mechi ya pili ili kusonga nusu fainali.

0 comments:
Post a Comment