Wednesday, April 15, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
Yanga na Azam zimekuwa zikibadilishana katika nafasi ya kwanza msimu huu, kabla ya wanajangwani kufanya vizuri katika mechi za karibuni huku Azam ikiambulia sare.'

MABINGWA watetezi Azam FC wamekumbana na nyakati ngumu baada ya leo kulazimishwa sare ya tatu mfululizo dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting Stars walipotoka 0-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, hivyo kuuweka rehani ubingwa kwa Yanga SC ambao wanahitaji kushinda mechi tatu tu kati ya tano zilizobaki ili wawe mabingwa.

Kwa matokeo hayo ya leo Azam FC sasa imefikisha pointi 39, saba nyuma ya vinara Yanga SC baada ya mechi 21. Yanga SC wakishinda mechi tatu kati ya tano zilizobaki, watafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote. Azam ikishinda mechi zake zote tano zilizobaki, itafikisha pointi 54.

Katika mechi tatu zijazo Yanga SC itachuana dhidi ya Polisi Moro FC, Ruvu Shooting Stars, Stand United FC, zote zitachezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakati Azam FC itacheza dhidi ya Stand United FC, Kagera Sugar FC na Simba SC, ambayo nayo inapigania kumaliza katika nafasi mbili za juu ili kushiriki michuano ya kimataifa.

Lakini, Yanga SC inaweza kutwaa ubingwa mapema zaidi endapo  itasimamishwa katika mechi hizo tatu ikiwamo dhidi ya Simba SC.

Kwa matokeo ya leo, Mgambo Shooting Stars inayonolewa na kocha mkuu mzawa, Bakar Shime, imepanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya sita hadi ya tano ikifikisha pointi 28 baada ya mechi 21.

Katika dakika ya 65 Azam FC imepata pigo kutokana kiungo wake Himid Mao kutolewa kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumkanyaga mshambuliaji Malimi Busungu. Mao ambaye ni mchezaji wa pili wa Azam kutolewa kwa kadi nyekundu msimu huu baada ya kiungo mwingine Salum Abubakar 'Sure Boy', ndiye aliyefunga bao la Azam katika sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar FC kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro Jumamosi.

Kabla ya kuikabili Mtibwa, Azam ilitoka kushikwa kwa sare nyingine ya 1-1 nyumbani Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam Jumatano ya wiki iliyopita dhidi ya Mbeya City FC.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video