
MABINGWA mara 24 wa ligi kuu Tanzania, Dar Young
Africans wamepaa kileleni kwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kufuatia
ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Mtibwa Sugar jioni hii katika mechi ya
ligi kuu iliyopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Kufuatia ushindi huo, Yanga wamefikisha pointi 25
kileleni baada ya kucheza mechi 13, na nyuma yao wamebaki mabingwa watetezi, Azam
fc wenye pointi 22 baada ya kucheza mechi 12.
Mabao ya Yanga leo hii yamefungwa kipindi cha pili
na mshambuliaji aliyekosa namba ya kudumu kikosini, Mrisho Khalfan Ngassa ‘Anko’.
Ngassa aliyetokea benchi alishangalia kwa
kuwashukuru mashabiki wa Yanga na alipofunga bao la pili alienda mpaka kwenye
benchi lao na kucheza na ‘Mwanaye’ Jerryson Tegete.
Winga huyu hatari hakuwahi kufunga katika mechi za
nyuma msimu huu na leo amefikisha idadi ya mabao mawili.
0 comments:
Post a Comment