Tuesday, February 17, 2015


Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, Yanga SC wataondoka nchini Alhamisi Februari 26 mwaka huu kwenda Gaborone, Botswana kwa ajili ya kurudiana na kikosi cha maafande wa BDF XI FC katika mechi ya pili ya hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.

Yanga SC inayokamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, itarudiana na timu hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Botswana mwishoni mwa wiki ijayo mjini Gaborone.

Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha ameuambia mtandao huu kuwa kikosi chao kitaondoka jijini hapa Alhamisi asubuhi kuwafuata maafande hao baada ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons FC (keshokutwa) na Mbeya City FC (Jumapili), mechi zote zikipigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

"Tutaondoka hapa Alhamisi ya wiki ijayo kuwafuata wapinzani wetu, tunaamini watacheza kwa kushambulia zaidi tofauti na walivyocheza hapa Dar es Salaam kwa kujilinda.

"Nasi tutaendelea kuwashambulia maana tunaamini mechi mbili za wiki hili zitatumika kumaliza ukame wa mabao katika safu yetu ya ushambuliaji," amesema Tiboroha mwenye PhD ya Sayansi ya Michezo.

Yanga SC ilishinda 2-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumamosi. Shukrani kwa mabao mawili ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Mrundi Amisi Tambwe.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video