Klabu ya Manchester United chini ya Kocha Mholanzi Louis Van Gaal, imekunwa na kiwango cha mchezaji wa klabu ya Fluminese Robert Kennedy kutoka nchini Brazil, ambapo sasa klabu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Old Trafford ipo tayari kutoa kiasi cha kitita Uro milioni Tano kumnasa mchezaji huyo.
Kennedy mwenye umri wa miaka Kumi na tisa amekuwa aking'ara akiwa na klabu yake ya Fluminese inayoshiriki Ligi kuu nchini Brazil na kiwango hicho kimeivutia klabu ya Manchester United kutaka Huduma za mchezaji huyo na uenda akajiunga na mashetani wekundu majira ya msimu wa joto.



0 comments:
Post a Comment