
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Uongozi wa Yanga SC umetamba kuwa kikosi chao kitaifumua mabao 10 moja ya timu watakayokutana nayo katika siku za karibuni.
Hayo yamesemwa muda mfupi uliopita na Katibu Mkuu wa klabu hiyo ya Jangwani jijini hapa, Dk. Jonas Tiboroha wakati akihojiwa na moja ya vituo vya redio jijini hapa.
Dk.Tiboroha amekiri kumekuwa na tatizo katika safu yao ya ushambuliaji, lakini limefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa ndiyo maana wamefunga mabao manne katika mechgi mbili zilizopita.
"Mechi mbili ambazo timu itacheza wiki hii jijini Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya City ni majaribio kwa timu yetu kabla ya kwenda Botswana kurudiana na BDF XI FC.
"Tumekuwa na ukame wa mabao kwa washambuliaji wetu katika mechi nyingi zilizopita, lakini makocha wamelifanyia kazi.
"Ipo siku Yanga itampiga mtu 10-0, ninaamini hilo kutokana na kikosi ambacho tunacho msimu huu," amesema zaidi Tiboroha mwenye PhD katika Sayansi ya Michezo.

0 comments:
Post a Comment