Tuesday, February 17, 2015


Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Mshambuliaji Said Bahanunzi wa Polisi Morogoro amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari wa Ligi Kuu Tanzania huku kiungo mkabaji Joseph Mahundi wa Coastal Union akishinda tuzo hiyo ya mwezi Desemba.

Baraka Kizuguto, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema jijini hapa leo kuwa wawili hao wamechaguliwa na jopo la makocha kutokana na mchango wao mkubwa kwenye timu zao katika mwezi husika.

Kizuguto amesema Mahundi anayeshikilia rekodi ya kufunga bao la mapema zaidi msimu huu, alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union mwezi Desemba mwaka jana. 

Hata hivyo, mabingwa hao wa 1988 wa Tanzania Bara, walicheza mechi moja tu Desemba wakitoka suluhu dhidi Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya Desemba 27, mwaka jana.

Ofisa Habari huyo ameendelea kueleza kuwa Bahanunzi, mfungaji bora wa Kombe la Kagame 2012 (mabao 6) anayechezea Polisi Moro FC kwa mkopo akitokea Yanga SC, amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake hiyo mpya tangu ajiunge nayo kwenye kipindi cha usajili cha dirisha dogo msimu huu.

Mwezi uliopita (Januari), Polisi Moro inayonolewa na Adolf Richard, ilikusanya pointi sita katika mechi nne, ikishinda 1-0 dhidi ya Mbeya City FC, sare dhidi ya Ndanda FC, Coastal Union FC na Stand United FC na kupoteza 1-0 dhidi ya Yanga SC.

Katika mechi hizo, Bahanunzi, mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar FC, alifunga mabao mawili yaliyowapa ushindi wa 1-0 nyumbani mjini Morogoro dhidi ya Mbeya City FC Januari 31 lililoipaisha timu yake hadi katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, na lile la sare ya 1-1 ugenini mjini Mtwara dhidi ya Ndanda FC Januari 10.

"Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi na Bahanunzi watazawadiwa fedha taslimu Sh. milioni moja kila mmoja kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo, Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Vodacom Tanzania," amesema Kizuguto.

Jopo maalum la makocha wanaotumwa kwenye viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za (VPL), ndilo linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi husika.

Tuzo hiyo imeanza kutolewa msimu huu. Wachezaji wengine waliowahi kuitwaa ni Antony Matogolo wa Mbeya City, ambaye kwa sasa anakipiga kwa mkopo Panone FC ya Kilimanjaro (Septemba), Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam FC (Oktoba) na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar FC (Novemba)

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video