
MAAFANDE wa Ruvu Shootings wa Mkoani Pwani
wanatarajia kuchuana na Red Arrows ya Zambia katika mechi ya kirafiki ya
kimataifa itayopigwa jumapili ya wiki hii uwanja wa Karume, jijini Dar es
salaam.
Afisa habari wa Shootings, Masau Bwire
amethibitisha kuwepo kwa mechi hiyo na amesema itaanza majaira ya saa 10:00
jioni.
“Mchezo huo utaanza saa 10 jioni, usipange kukosa,
utapitwa na burudani ya aina yake ambayo kuipata tena itakuchukua muda mrefu”.
Amekaririwa Bwire.
Red Arrowa FC ambayo ilitua jijini hapa jana, itamenyana na maafande hao wa Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Zambia.
Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema uongozi wa Red Arrows chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso Chilando ulifika wiki iliyopita makao makuu ya TFF sambamba na Ofisa habari wa klabu, Melody Siisii, Alex Chila ofisa ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kujitambulisha uwapo wao nchini.
Alhamisi ya wiki hii, Ruvu Shootings watakabiliana na Azam fc uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, katika mechi ya kiporo ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Wakati huo huo, Tanzania Prisons watakuwa nyumbani kwao Sokoine, Mbeya, kuonesha cheche na Yanga ya Dar es salaam.

0 comments:
Post a Comment