Thursday, February 19, 2015

TIMU mbili za Azam fc, Yanga, zinazochuana kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara zinashuka dimbani leo kusaka pointi tatu muhimu.
Vinara Azam fc wapo ugenini uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani kukabiliana na wenyeji wao Ruvu Shootings, wakati Yanga nao wapo ugenini Sokoine Mbeya kuchuana na Tanzania Prisons.
Azam wanaongoza ligi wakijikusanyia pointi 25 sawa na Yanga wanaoshika nafasi ya pili , lakini Wanalambalamba wana faida ya magoli mengi ya kufunga.
Matajiri hao wa jiji la Dar wamefunga magoli 22 na kufungwa 12, hivyo tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 10.
Yanga wamefunga magoli 15 na kufungwa magoli 7, tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ni 8.
Timu zote mbili zimeshuka dimbani mara 13.
Kama Yanga wanahitaji kupanda kileleni mwa ligi kuu wanatakiwa kushinda mechi ya leo na kuwaombea Azam fc wapigwe au washinde goli 1-0, halafu wao washinde 4-0.
Kama Yanga atapata ushindi huo atafikisha pointi 28 sawa na Azam watakaokuwa wamefikisha pointi 28 pia, lakini Yanga watakuwa wamefunga magoli 19 na kufungwa 7, hivyo tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa itakuwa 12.
Azam kama itatokea wamepata ushindi wa 1-0 wataendelea kuwa na pointi 28, magoli 23 ya kufunga na 12 ya kufungwa, tofauti ya itakuwa magoli 11.
Ikitokea mazingira hayo, Yanga watakwea kileleni mwa ligi kuu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video