
Akizungumza kuelekea mchezo huu Kocha wa City Juma Mwambusi amesema kuwa anafahamu uzito wa mechi hiyo hasa ukizingatia matokeo yaliyokuwepo msimu uliopita baina ya timu hizo hivyo kwa namna yoyote mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa City itacheza ikiwa na shauku ya kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa mzunguko wa pili msimu uliopita.
“Huu utakuwa ni moja ya michezo migumu tutaingia uwanjani tukiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wetu wa pili dhidi yao msimu uliopita, tulianza ligi vibaya msimu huu hasa katika michezo saba ya mwanzo, mara hii tuko vizuri ndiyo maana tuliweza kuifunga Simba nyumbani,najua utakuwa mchezo mgumu lakini matokeo ndiyo kitu pekee tunachokihitaji hivi sasa” alisema
Akiendelea zaidi Mwambusi alisema kuwa City imekuwa nje ya jiji la Mbeya takribani wiki nne ikicheza michezo ya ligi na kufanikiwa kushinda mmoja, ikitoka sare miwili na kupoteza mmoja jambo ambalo limewafanya wachezaji kuwa na ari kubwa ya kutafuta matokeo kwenye mchezo wa jumapili.

“Wachezaji wote wako vizuri kila mmoja ana ari kubwa, tunataka kushinda mchezo huu ili kuwahakikishia mashabiki wetu kuwa hatukubahatisha kuifunga Simba kwenye uwanja wa Taifa” alisema Mwasapili.
0 comments:
Post a Comment