Saturday, February 14, 2015

MABINGWA wa Uganda, KCCA wameanza vyema michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuwalaza bao 1-0 mabingwa wa Cameroon, Cosmos De Batia jioni hii uwanja wa Taifa wa Mandela, uliopo Namboole, nje kidogo ya jiji la Kampala.
Bao la KCCA katika mechi hii ya raundi ya kwanza limefungwa dakika ya 82' kupitia kwa Warman Waswa.
Hata hivyo timu zote zilicheza kwa kiwango kinachofanana ambapo kipindi cha kwanza wastani wa kumiliki mpira ulikuwa asilimia 51 kwa wenyeji na 49 kwa Wacameroon.
Kipindi cha pili hali ya kumiliki mpira ilikuwa asilimia 50 kwa 50.
Licha ya kushinda KCCA walikuwa katika wakati mgumu kutokana na presha kubwa waliyokuwa nayo Cosmos.
Mchezo wa marudiano hakika utakuwa mkali kwani kila timu ina nafasi ya kufanya vizuri, tofauti ni kwamba KCCA wana mtaji wa goli moja.
Wakali hao wa ligi ya Uganda wanahitaji suluhu katika mechi ya marudiano kule Cameroon.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video